Natazama Kalvari
| Natazama Kalvari | |
|---|---|
| Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
| Album | Asifiwe Bwana Mungu (Vol 8) |
| Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) |
| Composer | Gabriel Kapungu |
| Views | 6,724 |
Natazama Kalvari Lyrics
- Nimekukosa Bwana, kwa moyo wote ninajuta kweli, kwa moyo wote
Roho yangu ina-yohuzunika ninapokuona ulivyokufa{ Natazama Kalvari (Bwana) ulivyotundikwa mtini (kweli)
Mwili wangu wanyong'onyea ulivyosulibiwa } *2 - Tena ni mimi Bwana, ni dhambi zangu ulizozifia, msalabani
Kifo cha aibu, kilikufika makusudi mimi, niokolewe - Kwenye kilima kile, walikusonya wakisema wote, asulibiwe
Kifo chako kwetu ni ukombozi wa mioyo yetu, na roho zetu - Unitulize Bwana, kwa mkono wako kwani ninatubu, makosa yangu
Naanguka kwako kifudifudi, ninaomba toba, kwa moyo wote