Login | Register

Sauti za Kuimba

Tumshukuru Mungu Lyrics

TUMSHUKURU MUNGU

@ Fortune Shimanyi

 1. Tumshukuru Mungu kwa ukarimu wa-ke (pia)
  Pia na wema wake kutupenda namna hii

  { Nitazame - nitazame mimi (kisha ) nawe jitazame } *2
  (waweza) kuwa umeo-na (kama) tuko tofauti sura
  Nna hata matendo ( yetu) ni tofauti kweli
  Lakini Mungu wetu - wala habagui
  Anatupenda sote - ni vyema kumshukuru

 2. Matendo yake hayachunguziki, Mungu wetu (kweli)
  Kweli hatupaswi kuyachunguza mambo haya
 3. Mawazo yetu sisi yana upeo wake (wala)
  Hatuwezi kujua siri za Mungu wetu
 4. Twapaswa kushukuru kwa vyote tulivyo navyo
  Kwani kila kitu tumepewa na Mungu pekee
Tumshukuru Mungu
COMPOSERFortune Shimanyi
CHOIRSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
ALBUMAsifiwe Bwana Mungu (Vol 8)
CATEGORYThanksgiving / Shukrani
MUSIC KEYE
TIME SIGNATURE2
4
SOURCETanga
 • Comments