Nani Utamtumikia
| Nani Utamtumikia | |
|---|---|
| Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
| Album | Asifiwe Bwana Mungu (Vol 8) |
| Category | Tafakari |
| Composer | Gabriel Nghonoli |
| Views | 6,103 |
Nani Utamtumikia Lyrics
{
Chagueni hivi leo mtakayemtumikia
Chagua utakayemtumikia ni nani
Lakini mimi na nyumba yangu, (lakini) mimi (na nyumba yangu)
lakini mimi na nyumba yangu, nitamtumikia Bwana } *2- Pengine mwenzangu, waitumikia miungu
Unapopata shida, wakimbilia tunguri,
Waisahau ahadi yako ya ubatizo - Pengine mwenzangu, waitumikia tamaa
Maisha yako yote yametekwa na mali
Waithamini mali badala ya Mungu wako - Mtumikie Mungu, mtegemee siku zote
Achana na miungu, waganga wa kienyeji
Kwani Mungu pekee ndiye muweza wa yote