Wewe ni Mungu
   
    
     
         
          
            Wewe ni Mungu Lyrics
 
             
            
- // u t a n g u l i z i //
 
 Sikia aa sikia Bwana,
 Sikia aa sikia Bwana sauti yangu
 Sikia aa sikia leo
 Sikia aa sikia Bwana sauti yangu.
 
 Hii sauti inabeba hisia zangu
 Zilizomo moyoni mwangu sikia Bwana sauti yangu
 
 Naeleza furaha niliyo nayo
 Na hamu ya kukushukuru sikia Bwana sauti yangu.
 
 Nakufunulia moyo wangu uko wazi,
 Nakumiminia, sifa na tenzi Mwenyezi,
 Napiga kelele usikie Bwana sauti yangu
 
 Sikia aa sikia Bwana ( Mungu we)
 Sikia aa sikia Bwana sauti ya moyo,
 Moyo,moyo, wangu moyo, moyo, moyo ha ha-
 
 // k i i t i k i o //
 Nimejua ya kwamba - wewe ni Mungu kila wakati
 Naona wazi kwamba - wewe ni Mungu kila wakati
 Kwenye furaha - wewe ni Mungu kila wakati
 Na kwenye magumu bado- wewe ni Mungu kila wakati
 Haupungui neno - wewe ni Mungu kila wakatii
 // m a s h a i r i //
- Hukutaka raha zinipe kiburi -
 aeee eee ukanipimia.
 Na taabu ziliponishambulia - -
 ukafungua (Bwana) mlango nikatoka salama.
- Na vipaji ona hukunipa vyote -
 aaee eee ukanipimia.
 Ingawaje nilipoweka juhudi -
 ukafungua( Bwana) mlango nikatoka salama.
- Sikuumbwa msafi kama ulivyo,
 aaee eee ukanipimia.
 Hata hivyo dhambi iliponisonga,
 ukafungua ( Bwana) mlango nikatoka salama.
 
 // h i t i m i s h o //
 
 Yeyeyeye yeyeyeyeye yeyeyeyeyeeeeee
 
 Nakuja nimebeba sifa kukuzungushia
 Maana utukufu ni wako milele na milele-
 Nakuja nimebeba sifa kukuzungushia
 Maana utukufu ni wako milele na milele.
 
 Nakuja nimebeba shangwe, na chereko
 Nakuja nimebeba kinanda watu wakuimbie-
 Nakuja nimebeba sifa kukuzungushia
 Maana utukufu ni wako milele na milele.
 
 Nakuja nimebeba sifa kukupamba
 nakuja nimebeba maua jama watu wakutukuze-
 Nakuja nimebeba sifa kukuzungushia
 Maana utukufu ni wako milele na milele.
 
 Milele na milele, milele na milele,
 milele na milele,milele ni Mungu wa pekee...*5
 
 * (Bass) Wewe ni Mungu, wewe ni Bwana,
 we ni mwema, utabaki Mungu X2
 * ( Tenor) wewe ni wa kwanza ni Mungu weee, wewe ni wa mwisho eee
 Unaitwa Alfa ni Mungu wee, wewe ni Omega eee
MILELE NI MUNGU WA PEKEEEEEEE