I Love You
   
    
     
         
          
            I Love You Lyrics
 
             
            
- Siku tuliyoingoja mimi na wewe,
 Kwa uwezo wake mungu leo imefika,
 Popote uendapo tutakuwa pamoja
 {Mungu ametuunganisha mimi nawe,
 nasi wawili tena ni mwili mmoja,
 wewe ni wangu kweli
 na mimi ni wako njoo,
 I love you mpenzi wangu
 I need you siku zote I love you) *2
- Kwa maombezi yake mama yetu maria,
 Ahadi yetu sasa kweli imetimia,
- Chaguo la moyo wangu mimi nakupenda,
 Tulizo la moyo wangu njoo karibu yangu,
- Nimekuchagua wewe wangu wa maisha,
 Agizo la moyo wangu njo tujitulize,
- Mpenzi wangu nakupenda nawe unipende,
 Kwa penzi la raha na karaha tupendane,