Apewe Sifa
Apewe Sifa Lyrics
- { Sifa na utukufu vyote ni kwa Mungu hee heee
Sifa na utukufu vyote ni kwa Mungu hee hee } *2
{ Utukufu nakupa wewe, utukufu nakupa wewe,
Sifa na heshima nakupa we,
Ewe mwenyezi unaweza } *2
- Nguzo ya moto aliwasha, nilindwe usiku,
Nayo ya wingu akashusha nipite mchana
Nakumbuka mapito yote, niliyopitia,
Nakumbuka na njia zote, nilizopitia
Tazama Mungu tazama wewe,
Tazama Mungu tazama wewe
Tazama Mungu tazama wewe unatimiza ahadi yako
Tazama Mungu tazama wewe,
(tazama Mungu ) ni mwaminifu
Tazama Mungu tazama wewe unatimiza ahadi yako
Utukufu nakupa . . .
- Jemedari mwenye maguvu, yule Goliathi,
Akamlaza kwa kombeho, mkononi mwangu
Nakumbuka alikemea, mawimbi ya maji,
Nakumbuka yalimtii, nikafika ng'ambo
Tazama Mungu tazama . . .
Utukufu nakupa . . .
~ ~ ~
a) Bahari haiwezi kutuzuia -
Tunatembea bila mitumbwi
Na maji yanageuka kuwa ukuta -
Mungu mwenyewe ni mtumbwi wetu tunavuka
b) Maana amesema tumfuate -
Mizigo itulemeayo tukampe -
c) Muhimu tumwendee tukiamini -
Na hata juu ya maji tutakanyagaa -
~ ~ ~
{ Alimkumbuka Daudi mtumishi wake
Akamkweza akawavusha waisrael
katika maji bila mitumbwi } *2
Apewe, apewe, apewe sifa kuu
Mungu apewe, apewe, milele milele
Apewe apewe, apewe sifa kuu
Mungu apewe, apewe
Sifa na utukufu vyote ni kwa Mungu hee hee