Kipenzi Changu

Kipenzi Changu
Performed bySt. Joseph Migori
CategoryHarusi
ComposerAfred Ossonga
Views12,048

Kipenzi Changu Lyrics

 1. { Wewe ni kipenzi changu, wewe ni kizuri changu
  Tulizo la moyo wangu, chaguo langu
  Nitaishi nawe daima, nitakufuata popote
  Utakapokwenda tutatembea pamoja (pamoja nawe)} *2

 2. Nakupenda ee mwenzangu, nimekupa pendo langu
  Nawe nipe penzi lako kwa moyo wote } *2
 3. Jina langu ni kipenzi, jina lako kitulizo,
  Njoo tukajitulize mimi na wewe } *2
 4. Nakuita ee mwenzangu, nakuita njoo kwangu
  Njoo nikupe agizo la moyo wangu } *2
 5. Siondoki kando yako, siondoke kando yangu
  Kifo ndicho kitakachotutenganisha } *2