Login | Register

Sauti za Kuimba

Kipenzi Changu Lyrics

KIPENZI CHANGU

@ Afred Ossonga

{ Wewe ni kipenzi changu, wewe ni kizuri changu
Tulizo la moyo wangu, chaguo langu
Nitaishi nawe daima, nitakufuata popote
Utakapokwenda tutatembea pamoja (pamoja nawe)} *2

 1. Nakupenda ee mwenzangu, nimekupa pendo langu
  Nawe nipe penzi lako kwa moyo wote } *2
 2. Jina langu ni kipenzi, jina lako kitulizo,
  Njoo tukajitulize mimi na wewe } *2
 3. Nakuita ee mwenzangu, nakuita njoo kwangu
  Njoo nikupe agizo la moyo wangu } *2
 4. Siondoki kando yako, siondoke kando yangu
  Kifo ndicho kitakachotutenganisha } *2
Kipenzi Changu
COMPOSERAfred Ossonga
CHOIRSt. Joseph Migori
CATEGORYHarusi
MUSIC KEYA
TIME SIGNATURE2
4
 • Comments