Niruhusu ee Yesu
Niruhusu ee Yesu Lyrics
Niruhusu Yesu wangu, niijongee meza yako
Unisamehe dhambi Mwokozi,
uje rohoni mwangu uniokoe
Njoo kaa ndani yangu, nami nikae ndani yako
Ili nipate amani tele, ndani ya Roho yangu nifarijike
{ Wewe Bwana (wewe Bwana wanijua)
Wanijua (hata nafsini mwangu)
Wewe ndiwe tabibu pekee wa roho yangu
Tena ndiwe kimbilio langu }*2
- Tazama Yesu wangu ninajongea karamu yako
Pengine kwako Bwana sikustahili kuijongea
Unihurumie ee Yesu wangu unisamehe
- Hakika kwako Bwana makosa mengi nimeyatenda
Ubinadamu wangu siwezi kuficha kwako Bwana
Unihurumie ee Yesu wangu unisamehe
- Niwazi Yesu wangu unaujua udhaifu wangu
Sina chakujitolea mbele yako Ee Yesu wangu
Unihurumie Ee Yesu wangu unisamehe