Nusu kwa Nusu
Nusu kwa Nusu Lyrics
- Ni yule yulee
Ni yule yulee
Ni yule yulee
Mungu alivyo ooh hivyo ndivyo alivyo,
Mungu alivyo ooh hivyo ndivyo alivyo,
Mchana ni yule yule ( na ) usiku ni yule yule,
(Yeye) habadiliki ni yule, daima ni yule yule,
( ye ni yule Mungu) Mungu alivyo ooh
Hivyo ndivyo alivyo ndivyo alivyo
- Alifundisha upendo akawafia wadhambi
Kahubiri msamaha kaombea wauaji
Anahimiza amani hata kwa wanaomkamata
Kweli Mungu habadiliki (yeye) ni yule yulee
- Kaagiza ubatizo akabatizwa mwenyewe
Alihubiri huruma akawaponya wakoma
Anahimiza ibada naye hakutegea kusali
Kweli Mungu habadiliki (yeye) ni yule yulee
~ ~ ~
Lakini mwanadamu mimi- Mwanadamu mimi ni nusu kwa nusu *2
Nahubiri upendo - Mwanadamu mimi ni nusu kwa nusu
Huku nateta wenzangu - Mwanadamu mimi ni nusu kwa nusu
Nataka msamaha - Mwanadamu mimi ni nusu kwa nusu
Huku nashitaki watu - Mwanadamu mimi ni nusu kwa nusu
Natangaza amani - Mwanadamu mimi ni nusu kwa nusu
Huku nabeba silaha - Mwanadamu mimi ni nusu kwa nusu
Navaa msalaba - Mwanadamu mimi ni nusu kwa nusu
Na hirizi kiunoni - Mwanadamu mimi ni nusu kwa nusu
Nina pete ya ndoa - Mwanadamu mimi ni nusu kwa nusu
Na hawara mafichoni - Mwanadamu mimi ni nusu kwa nusu
Napaswa kugeuka - Mwanadamu mimi ni nusu kwa nusu
Niwe mwenye msimamo - Mwanadamu mimi ni nusu kwa nusu
Maana mwanadamu mimi - Mwanadamu mimi ni nusu kwa nusu *3