Maneno Tu
Maneno Tu Lyrics
- Hohohohoho maneno hohohohoho maneno tu *2
Hoo hoo maneno ohoo bila matendo x2
Nampenda Mungu ( maneno tu )
Nampenda Mungu (maneno tu) hayooooo
- Kutwa kucha maneno tu familia yako inayumba amani imetoweka hiyo..
Umeitelekeza unaponda mali kwa anasa huna wasiwasi,
Umeiangamiza unaponda mali weee- eti nampenda Mungu eeh, ehee, maneno tu
- Kutwa kucha maneno tu hupatani na jirani yako hata salamu hampeani,
Matatizo yake wayashabikia kwa furaha huna wasiwasi,
Nazo shida zake wazishangilia weee - eti nampenda Mungu eeh,ehee,maneno tu
- Kutwa kucha maneno tu madaraka yako ni ya uma, unayafuja unavyopenda,
Hauwajali watu wanaoteseka waliao huna wasiwasi
Hauwajali watu wanaoumia weee - eti nampenda Mungu eeh,ehee,maneno tu
~ ~ ~
Tena nampenda Mungu wangu- nampenda nampenda kuliko kitu chochote
Na jirani yangu nampenda- nampenda kama nafsi yangu.
Ni amri ya Mungu( tena) ndiyo amri kuu,
lakini matendo yako hayafanani na maneno,
unang'ara uso wako, moyoni unang'ata meno,
Tazama, matendo, matendo yako, tazama mwenendo, mwenendo wako( aiyooo)
Ndugu acha maneno,( ooh hayoo) maneno tu,
Upendo ni matendo (na kabisa ni) matendo
Ndugu acha maneno (ooh acha) maneno tu,
Upendo ni matendo ( na kabisa ni ) matendo *2