Makao Yetu
Makao Yetu | |
---|---|
Alt Title | Wewe Bwana Umekuwa Makao Yetu |
Performed by | St. Kizito Makuburi |
Album | Mimina Neema |
Category | Zaburi |
Composer | E. F. Jissu |
Views | 18,227 |
Makao Yetu Lyrics
{ Wewe Bwana umekuwa, makao yetu sisi,
kizazi baada ya Kizazi } *2
{ Kabla haijazaliwa milima (milima yote)
Wala haujaiumba dunia ( dunia yote)
Na tangu milele yote, ndiwe Mungu } *2- Wamrudisha, mtu mavumbini, usemapo,
Rudini, rudini, rudini enyi wanadamuuu. - Maana miaka, elfu machoni pako, ni kama siku,
Siku ya jana, ikiisha, kupita, na kama kesha la usikuuu. - Wawagharikisha, huwa kama usingizi eehee,
Asubuhi huwa kama majani yameayo, asubuhi,
Huchipuka na kumea, jioni yakatika,(jioni) na kukaukaaa.
~ ~ ~
Na uzuri wa Bwana - ohooo uzuri wa Bwana
Na uzuri wa Bwana - eeheee uzuri wa Bwana
Bwana Mungu wetu uwe juu yetu - oohooo uwe juu yetu
{ Na kazi ya mikono yetu ee Mungu uithibiti - eeheeee uithibitishe,
Utufanyie fanyie thabiti -
kazi ya mikono naam kazi ya mikono yetu uithibitishe } *2