Makao Yetu Lyrics

MAKAO YETU

@ E. F. Jissu

{ Wewe Bwana umekuwa, makao yetu sisi,
kizazi baada ya Kizazi } *2
{ Kabla haijazaliwa milima (milima yote)
Wala haujaiumba dunia ( dunia yote)
Na tangu milele yote, ndiwe Mungu } *2

 1. Wamrudisha, mtu mavumbini, usemapo,
  Rudini, rudini, rudini enyi wanadamuuu.
 2. Maana miaka, elfu machoni pako, ni kama siku,
  Siku ya jana, ikiisha, kupita, na kama kesha la usikuuu.
 3. Wawagharikisha, huwa kama usingizi eehee,
  Asubuhi huwa kama majani yameayo, asubuhi,
  Huchipuka na kumea, jioni yakatika,(jioni) na kukaukaaa.

  ~ ~ ~

  Na uzuri wa Bwana - ohooo uzuri wa Bwana
  Na uzuri wa Bwana - eeheee uzuri wa Bwana
  Bwana Mungu wetu uwe juu yetu - oohooo uwe juu yetu
  { Na kazi ya mikono yetu ee Mungu uithibiti - eeheeee uithibitishe,
  Utufanyie fanyie thabiti -
  kazi ya mikono naam kazi ya mikono yetu uithibitishe } *2
Makao Yetu
ALT TITLEWewe Bwana Umekuwa Makao Yetu
COMPOSERE. F. Jissu
CHOIRSt. Kizito Makuburi
ALBUMMimina Neema
CATEGORYZaburi
REFZab 90: 1-2
MUSIC KEYE
TIME SIGNATURE6
16
SOURCETanga
 • Comments