Login | Register

Sauti za Kuimba

Nyota ya Mashariki Lyrics

NYOTA YA MASHARIKI

@ Bernard Mukasa

 1. Kakukirimia, uwe ulivyo,
  Atakutumia impendezavyo
  Akikuinua, inuka, hivyo,
  Ninakuombea heri vilivyo;

  Hakunipa hayo, nikuhitaji,
  Kwa niliyo nayo, upate maji,
  Na mwisho wa hayo, tuvikwe taji,
  Tuingie nayo, wa mbingu mji.

  { Nimeiona nyota yako mashariki (nyota yako)
  Ninajivuna inavyong'ara rafiki (helelelele)
  Naandamana kuja unakotamalaki
  Kumsujudia Bwana aliyekupa milki (ho ndugu) } *2

 2. Sirudi kwa njia, yake herode,
  Anakuvizia, kila upande,
  Wivu unamjia, kakunja, konde,
  La kukuzuia juu usipande;

  Ni kama Kaini, mwua Abeli,
  Au Raubeni, wa Israeli,
  Waliotamani, kuzika, hali,
  Ya wadogo duni, wake Jalali!
 3. Ninakuombea, usife moyo,
  Maana dunia, si rafikiyo,
  Wewe fuatia, za Kristu, nyayo,
  Aliyekufia, kwa mizigoyo;

  Wa ulimwenguni, watakufumba,
  Wazuri machoni, moyo mwembamba,
  Hawatatamani, uitwe, mwamba,
  Ni wivu moyoni, unawasomba!
Nyota ya Mashariki
COMPOSERBernard Mukasa
CHOIRSt. Kizito Makuburi
ALBUMMimina Neema
CATEGORYTafakari
SOURCEDar-es-Salaam




 • Comments