Mungu ni Upendo
   
    
     
         
          
            Mungu ni Upendo Lyrics
 
             
            
- Mungu ni upendo, tupendane *4 ae ae
 
 Tufuateni upendo na kutaka karama za rohoni *2
 Lakini zaidi mpate mpate kutubu *2 ae ae
 { Nijaposema kwa lugha za wanadamu na malaika
 Mimi kama mimi sina upendo - nimekuwa shaba iliayo (mimi)
 Nijaposema kwa ndimi za wanadamu na malaika
 Mimi kama mimi sina upendo - nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao } *2
- Tena nijapokuwa na unabii,
 Na kujua siri zote na maarifa yote
 Nijapokuwa na imani kamilifu
 Kiasi cha kuweza kuhamisha milima
 Kama sina upendo, si kitu mimi!
 
 Tena nikitoa mali zangu zote, kuwalisha maskini
 Tena nikijitoa mwili wangu, niungue moto
 Kama sina upendo, si kitu mimi!
- Upendo huvumilia, hufadhili
 Upendo hauhusudu, hautakabari
 Upendo haujivuni, haujivuni
 
 Haukosi kuwa na adabu
 Hautafuti mambo yake
 Hauoni uchungu
 Hauhesabu mabaya
 Haufurahi udhalimu
 Bali hufurahi pamoja na ukweli
 Huvumilia yote
 Huamini yote
 Hutumaini yote
 Hustahimili yote
 
 Upendo upendo upendo ni kila kitu