Ni Neema
Ni Neema | |
---|---|
Alt Title | Neema za Mungu |
Performed by | Moyo Mtakatifu wa Yesu UDSM |
Album | Neema za Mungu |
Category | Thanksgiving / Shukrani |
Composer | Zacharia Gerald |
Views | 24,383 |
Ni Neema Lyrics
- Tunafanya kazi kwa juhudi na nguvu nyingi tena tunajituma
Mafanikio yake tunayaona wazi kwa macho yetu
Tunaridhika na kujiona tunafanya sisi
Kwa nguvu na akili zetu tunasahau ya kwamba hizi ni neema{ Ni neema (neema) mi neema (ni neema)
Ni neema (neema) zake mwenyezi } *2 Mungu - Na elimu tunapata kwa gharama kubwa tena elimu ya juu
Na tunadhani kwamba ni akili zetu za kibinadamu
Tunagundua vitu vipya bora na vya kisasa
Vya kuvutia eti tekinolojia yetu imekua wapendwa - Turudishe sifa utukufu na enzi kwa Mungu aliyetuumba
Na tuwe na hofu kwake kwani yeye anatupa yote
Tunayaweza yote katika yeye peke yake,
Tunayaweza haya yote ni kwa yeye atutiaye nguvu kweli
~ ~ ~
{ Piga vigelegele*3
Piga makofi piga vigelegele piga makofi }
Yeye ndiye nguvu yetu, Yeye ndiye ngao yetu
Yeye ndiye shibe yetu yeye ndiye Mungu wetu milele
{Piga makofi} *6
Piga vigelegele *3
Piga makofi *3