Ni Neema

Ni Neema
ChoirMoyo Mtakatifu wa Yesu UDSM
AlbumNeema za Mungu
CategoryThanksgiving / Shukrani
ComposerZacharia Gerald

Ni Neema Lyrics

 1. Tunafanya kazi kwa juhudi na nguvu nyingi tena tunajituma
  Mafanikio yake tunayaona wazi kwa macho yetu
  Tunaridhika na kujiona tunafanya sisi
  Kwa nguvu na akili zetu tunasahau ya kwamba hizi ni neema

  { Ni neema (neema) mi neema (ni neema)
  Ni neema (neema) zake mwenyezi } *2 Mungu

 2. Na elimu tunapata kwa gharama kubwa tena elimu ya juu
  Na tunadhani kwamba ni akili zetu za kibinadamu
  Tunagundua vitu vipya bora na vya kisasa
  Vya kuvutia eti tekinolojia yetu imekua wapendwa
 3. Turudishe sifa utukufu na enzi kwa Mungu aliyetuumba
  Na tuwe na hofu kwake kwani yeye anatupa yote
  Tunayaweza yote katika yeye peke yake,
  Tunayaweza haya yote ni kwa yeye atutiaye nguvu kweli

  ~ ~ ~
  { Piga vigelegele*3
  Piga makofi piga vigelegele piga makofi }
  Yeye ndiye nguvu yetu, Yeye ndiye ngao yetu
  Yeye ndiye shibe yetu yeye ndiye Mungu wetu milele
  {Piga makofi} *6
  Piga vigelegele *3
  Piga makofi *3