Kwa Nini Nisiende
Kwa Nini Nisiende Lyrics
- Na nyumbani mwake Bwana, nani ataingia
Bwana yuko mlangoni, atungoja tuingie
Twendeni wote kwake, tumtolee ibada kweli
Kwa nini nisiende (nyumbani) *2
Niingie nyumbani mwake
Kwa nini nisiende (nyumbani) *2
Nishiriki karamuye
Kwa nini nisiende (nyumbani) *2
Nimshukuru Muumba wangu
- Kina baba tuingie, kina mama tuingie
Tukamuimbie Bwana, nyimbo nzuri za furaha
- Vijana tuingie, na watoto tuingine
Tukamuimbe Bwana, nyimbo nzuri za furaha
- Makasisi tuingie, na watawa tuingie
Tukamuimbe Bwana, nyimbo nzuri za furaha
- Tupige vigele gele, kayamba ngoma tucheze
Kuruka pia turuke, shingo na zinesenese