Heri Mume Yule
   
    
     
        | Heri Mume Yule | 
|---|
| Performed by | - | 
| Category | Harusi | 
| Composer | Ochieng Odongo | 
| Views | 6,827 | 
Heri Mume Yule Lyrics
 
             
            
- Heri mume Yule, aliye na mke mwema x2.
 Siku za maisha yake, siku za maisha yake zitaongezwa tena maradufu x2
- Mke hodari humfurahisha mumewe, yeye ni tunu bora kutoka kwa Mungu.
- Mwenye huleta Baraka juu ya Baraka, hata huleta wema usio na bei.
- Mwenye rehema humpendeza mumewe, na maarifa yake yatamnenepesha.
- Kama ilivyo jua lipambazukavyo, ndivyo uzuri wa mke mwema ulivyo
 ivume sana mito ipige makofi *2.