Nitakutukuza Mungu
Nitakutukuza Mungu Lyrics
- Bwana viumbe vyote vilivyoumbwa nawe
Vinakutukuza kwa haki *2
Ona mimea nayo iliyoumbwa nawe
Inakutukuza kwa haki, inakutukuza Mungu
Uhimidiwe Baba yetu uhimidiwe
Uhimidiwe uhimidiwe
Uhimidiwe Baba yetu uhimidiwe
Uhimidiwe Mungu upewe sifa
- Bahari na vitu vyote viliyoumbwa nawe
Vinakuimbia kwa haki *2
Ona dunia yote iliyoumbwa nawe
Inakuimbia kwa haki, inakuimbia Mungu
- Bwana nikiyatazama matendo yako kwangu
Ninakutukuza kwa haki
Ninakutukuza ee Mungu
Ninakosa la kusema, ni mengi mno kwangu
Ninakushukuru ee Yesu, ninakushukuru sana
- Mfalme Daudi alikuchezea - uhimidiwe
Na mavazi yake kayararua - upewe sifa
Mimi ni nani nisikutukuze -uhimidiwe
Nitakuimbia ningali hai - upewe sifa
Wafalme nao wanakutukuza - uhimidiwe
Na majeshi yote yanakusifu - upewe sifa
Kwa kinywa changu napaza sauti - uhimidiwe
Na nyumba yangu wote tunasema - upewe sifa
Upewe sifa, upewe sifa *2
Nitakusifu milele milele (Baba) milele *8