Login | Register

Sauti za Kuimba

Nitakutukuza Mungu Lyrics

NITAKUTUKUZA MUNGU

@ Zacharia Gerald

 1. Bwana viumbe vyote vilivyoumbwa nawe
  Vinakutukuza kwa haki *2
  Ona mimea nayo iliyoumbwa nawe
  Inakutukuza kwa haki, inakutukuza Mungu

  Uhimidiwe Baba yetu uhimidiwe
  Uhimidiwe uhimidiwe
  Uhimidiwe Baba yetu uhimidiwe
  Uhimidiwe Mungu upewe sifa

 2. Bahari na vitu vyote viliyoumbwa nawe
  Vinakuimbia kwa haki *2
  Ona dunia yote iliyoumbwa nawe
  Inakuimbia kwa haki, inakuimbia Mungu
 3. Bwana nikiyatazama matendo yako kwangu
  Ninakutukuza kwa haki
  Ninakutukuza ee Mungu
  Ninakosa la kusema, ni mengi mno kwangu
  Ninakushukuru ee Yesu, ninakushukuru sana
 4. Mfalme Daudi alikuchezea - uhimidiwe
  Na mavazi yake kayararua - upewe sifa
  Mimi ni nani nisikutukuze -uhimidiwe
  Nitakuimbia ningali hai - upewe sifa
  Wafalme nao wanakutukuza - uhimidiwe
  Na majeshi yote yanakusifu - upewe sifa
  Kwa kinywa changu napaza sauti - uhimidiwe
  Na nyumba yangu wote tunasema - upewe sifa

  Upewe sifa, upewe sifa *2
  Nitakusifu milele milele (Baba) milele *8
Nitakutukuza Mungu
ALT TITLEUhimidiwe
COMPOSERZacharia Gerald
CATEGORYThanksgiving / Shukrani
 • Comments