Nikiziangalia Nchi
Nikiziangalia Nchi | |
---|---|
Performed by | St. Vincenti Palloti Makiungu Singida Tz |
Category | Thanksgiving / Shukrani |
Composer | Bernard Mukasa |
Views | 3,785 |
Nikiziangalia Nchi Lyrics
- Nimezitafakari habari za anga na maji
Nikainua macho yangu, kuitazama nchi kavu
Na miondoko ya viumbe wote waliomo
Sauti zao na tamaduni zaoNikiziangalia nchi na pande zake zote
Nikiitazama milima na mabonde yote
Utukufu wako nakupa Mungu wangu
Sifa na heshima
Utukufu wako nakupa Mungu wangu
Na enzi ni yako
Utukufu wako nakupa Mungu wangu
Daima milele
Utukufu wako nakupa Mungu wangu - Wanyama juu ya anga na ndege wote angani
Samaki nao baharini na mimea ya ardhini
Wote umetoa wewe uhai ukaanza
Dunia yote ikawa furaha - Ili kuondoa upweke ukaanzisha lugha
Viumbe tuwasiliane tupate kukamilishana
Upendo gani huu kwa tusioweza shukuru
Ingawa tunafurahia kupendwa - Unafahamu shida zetu na mahitaji yetu
Mipango yetu ya maisha daima unainyoosha
Ingawa macho yetu hayajawahi kukuona
Lakini daima hautusahau - Ningetamka moja moja sifa zako Mwenyezi
Lakini ni nyingi sana na akili yangu inaganda
Nabaki kutabasamu ninapokukumbuka
Halafu ninaimba wimbo wa shangwe