Nikiziangalia Nchi

Nikiziangalia Nchi
ChoirSt. Vincenti Palloti Makiungu Singida Tz
CategoryThanksgiving / Shukrani
ComposerBernard Mukasa

Nikiziangalia Nchi Lyrics

 1. Nimezitafakari habari za anga na maji
  Nikainua macho yangu, kuitazama nchi kavu
  Na miondoko ya viumbe wote waliomo
  Sauti zao na tamaduni zao

  Nikiziangalia nchi na pande zake zote
  Nikiitazama milima na mabonde yote
  Utukufu wako nakupa Mungu wangu
  Sifa na heshima
  Utukufu wako nakupa Mungu wangu
  Na enzi ni yako
  Utukufu wako nakupa Mungu wangu
  Daima milele
  Utukufu wako nakupa Mungu wangu

 2. Wanyama juu ya anga na ndege wote angani
  Samaki nao baharini na mimea ya ardhini
  Wote umetoa wewe uhai ukaanza
  Dunia yote ikawa furaha
 3. Ili kuondoa upweke ukaanzisha lugha
  Viumbe tuwasiliane tupate kukamilishana
  Upendo gani huu kwa tusioweza shukuru
  Ingawa tunafurahia kupendwa
 4. Unafahamu shida zetu na mahitaji yetu
  Mipango yetu ya maisha daima unainyoosha
  Ingawa macho yetu hayajawahi kukuona
  Lakini daima hautusahau
 5. Ningetamka moja moja sifa zako Mwenyezi
  Lakini ni nyingi sana na akili yangu inaganda
  Nabaki kutabasamu ninapokukumbuka
  Halafu ninaimba wimbo wa shangwe