Mtume
Mtume |
---|
Alt Title | Nitamwimbia Bwana Milele |
Performed by | - |
Category | Tafakari |
Composer | Bernard Mukasa |
Views | 9,339 |
Mtume Lyrics
- Dunia hii ni ngumu sana
Yenye mapito mazito
Siku zote watu kulumbana
Kote kote kuna moto
Ooo ni vigumu mno
Ooo kuwajibika
Kwa aliyekutuma
Lakini mimi, tazama
Nimeinua macho yangu
Nimtazame mmoja
Yeye ni rafiki yangu
Kisiwa cha faraja
Mimi ni mtume wake
Mtume wa uimbaji
Ninaimba nyimbo zake
Kwa wanaomhitaji Yesu
- Duniani kumejaa wivu
Ugombea utukufu
Hasira kali zao wavivu
Watukuzao upofu
Ooo wanaumiza
Ooo wanavunja moyo
Wakatiza tamaa
Lakini mimi, tazama
- Duniani kumbe siyo kwangu
Nimetumwa kwa muda tu
Nifanye kazi ya Bwana wangu
Nimalize notoke tu
Ooo nitaitimiza
Ooo nimeamua
Nikavalishwe taji
Milele mimi, tazama
- Uchovu usingizi uvivu
Na umaskini wangu
Siruhusu vinitege nyavu
Nishike utume wangu
Ooo ninakaza mwendo
Ooo sirudi nyuma
Sitamwangusha Yesu
Milele mimi tazama
~ ~ ~
Kwa wanaomhitaji Yesu
Nyimbo zake - kwa wanaomhitaji Yesu
Habari zake - kwa wanaomhitaji Yesu
Na kazi zake - kwa wanaomhitaji Yesu
Mimi nayo nyumba yangu - nitamwimbia Bwana milele
Na waimbaji wenzangu - nitamwimbia Bwana milele
Mimi na rafiki zangu - nitamwimbia Bwana milele
Ndugu na rafiki zangu - nitamwimbia Bwana milele
Nitamwimbia Bwana milelee