Safari ni Moja

Safari ni Moja
Performed by-
CategoryGeneral
ComposerBernard Mukasa
Views3,974

Safari ni Moja Lyrics

  1. Twajua Mbingu iko mbali na njia ndefu,
    tena mitego ni mingi kila kona,
    lakini tumaini liko karibu nasi,
    kwamba Yesu alikufa kwa ajili yetu,
    Naye atatuongoza tukimwamini,
    mpaka tufike salama tuendakoo.

    Safari ni moja tena na njia ni moja (aa)
    Hatua ni moja moja foleni ni moja(naa)
    Mlango mmoja tena mlango mwembamba,
    (twendee) twende tuingie tukaishi huko milele *2
  2. Shetani hakuanza leo kutuvuruga,
    tangu pale kwenye mti bustanini,
    kavunja ujamaa mwema wa Babu zetu,
    wakamkosea Mungu Wakaanguka,
    nao wakajihukumu wakajificha,
    wakitaka wapotee mbali naye.
  3. Ya Mbingu yakajinyenyekeza duniani,
    Laana ikatakaswa kwa sadaka,
    ya mti yakavunjwa vunjwa juu ya mti,
    ya bustanini yakashindwa mlimani,
    aibu ya Mwanadamu ikaondoka,
    akaandaliwa Ufalme Mbinguni.

    T/B: Tutazame mbele na tusigeuke nyuma,
    Mwokozi wetu Yesu Anatungojea.

    Wote: Safari ni moja safari moja,
    Twendeeni pamoja safari moja,
    Ipande milimani ni moja safari moja,
    Ishuke Mabondeni ni moja safari moja,
    Inyeshe liwake ni moja safari ni moja tuu.