Tumaini Jema
Tumaini Jema |
---|
Performed by | - |
Category | General |
Composer | Bernard Mukasa |
Views | 2,937 |
Tumaini Jema Lyrics
- Hawataaibika, wala hawatafedheheka
Milele na milele (milele) wao watashinda magumu
Radi haitawapiga, mvua haitawagharikisha
Milele na milele (milele) wao watashinda mauti
Tazama
Hawa ndio wale waliotambua (kuwa)
Bwana Yesu ndiye fimbo ya ushindi (tena)
Na wakakubali kumtumainia (yeye)
Yesu ni mwamba na yeye mshindi (ni)
Yesu kamanda wa wote tumwende yeye
- Wamtumainiao, wamechagua fungu jema
Kwani hawatakwama wala kushindwa na lolote
- Yesu aliahidi, kutoa kila aombwapo
Naye ni mwaminifu, anayetimiza ahadi
- Kuugua kufiwa, si tatizo kwa watu hawa
Ufukara si hoja, kwa wamtumainiao Yesu
- Vita wameshavishinda, mapambano wamemaliza
Na wamevikwa taji, wamevikwa taji la haki