Tumaini Jema

Tumaini Jema
ChoirTBA
CategoryGeneral
ComposerBernard Mukasa
Musical Notes
Time Signature6
16
Music KeyG

Tumaini Jema Lyrics

 1. Hawataaibika, wala hawatafedheheka
  Milele na milele (milele) wao watashinda magumu
  Radi haitawapiga, mvua haitawagharikisha
  Milele na milele (milele) wao watashinda mauti

  Tazama
  Hawa ndio wale waliotambua (kuwa)
  Bwana Yesu ndiye fimbo ya ushindi (tena)
  Na wakakubali kumtumainia (yeye)
  Yesu ni mwamba na yeye mshindi (ni)
  Yesu kamanda wa wote tumwende yeye
 2. Wamtumainiao, wamechagua fungu jema
  Kwani hawatakwama wala kushindwa na lolote
 3. Yesu aliahidi, kutoa kila aombwapo
  Naye ni mwaminifu, anayetimiza ahadi
 4. Kuugua kufiwa, si tatizo kwa watu hawa
  Ufukara si hoja, kwa wamtumainiao Yesu
 5. Vita wameshavishinda, mapambano wamemaliza
  Na wamevikwa taji, wamevikwa taji la haki

Favorite Catholic Skiza Tunes