Fumbueni Vinywa
Fumbueni Vinywa Lyrics
- { Fumbueni vinywa vyenu (fumbueni) mkapaze sauti zenu
mkisifu mkishangilia ukuu wa Bwana Mungu wetu
Mkirukaruka huku mkiimba sifa za Bwana Mungu wetu } *2
{ Pazeni sauti (pazeni sauti) mkiimba kwa furaha
Fanyeni shangwe kwa zaburi ngoma hata na matari } *2
- Tukuzeni sifa zake, tukuzeni sifa zake,
imbeni imbeni zaburi imbeni zaburi
Pigeni kelele za shangwe kwa furaha
Msifuni Mungu wenu kwa kinanda na kinubi
- Kwa maana kusifu kwapendeza, kusifu kwapendeza
Basi njooni tumsifu Bwana Mungu wetu