Lo Ajabu Kupata Uzima
Lo Ajabu Kupata Uzima | |
---|---|
Alt Title | And Can It Be |
Performed by | Sauti Tamu Melodies |
Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) |
Composer | Charles Wesley |
Video | Watch on YouTube |
Views | 7,813 |
Lo Ajabu Kupata Uzima Lyrics
- Lo! Ajabu kupata uzima,
Katika damu ya Mwokozi wangu
Aliyenifia pendoni
Mimi niliyemsulubisha
Upendo huu wa kushangaza kabisa
Wewe Yesu wangu kunifia pendoni
{ Upe - upendo huu,
Nashaa- nashangaa,
Yesu - Yesu wangu kunifilia } * 2 - Yesu wangu alitoa damu
Siwezi kuelewa neno hili
Viumbe vyote vya Mbinguni
Navyo haviwezi kufahamu
Najua tu ni kwa rehema zake Mungu
Malaika watu wote wamsujudu mno
{ Ni re - ni rehema
Tumwa - tumwabudu
Tumwa - tumwamini ndiye Mwokozi } * 2 - Aliondoka kule mbinguni
Kwa nyumba yake Mungu Baba yake
Na utukufu aliacha
Afe kwa ajili ya maovu
Rehema zake ni nyingi na ukarimu
Kwani Mungu wangu aliniokoa mimi
{ Sista - sistahili
Neema - neema zake
Laki - lakini alinioka } * 2 - Roho yangu ilifungwa sana
Dhambi na giza vilinilemea
Akaniangaza rohoni
Gereza langu likang'aa mno
Ikafunguka minyororo yangu yote
Nikaondoka nikaanza kumfuata
{ Siku - siku ile
Nika - nikapata
Uhu - uhuru kweli kwake Mungu } * 2 - Hukumuni mimi simo sasa
Mimi ni wake Yesu ndiye wangu
Yeye ni kichwa changu kweli
Na amenivika haki yake
Mimi hodari sasa kwa kiti cha enzi
Napewa taji ya milele katika Yesu
{ Sina - sina hofu
Kuso - kusogea
Kati - katika Bwana wangu Kristo } * 2