Mizinga Maroketi

Mizinga Maroketi
Performed bySt. Kizito Makuburi
AlbumMungu Yule
CategoryTafakari
ComposerCharles Ruta
Views641

Mizinga Maroketi Lyrics

  1. Amani ya dunia imetoweka
    Tumuombe Mwenyezi aturudishie
    Tamaa ubinafsi vilivyoshamiri
    Ni sumuyo amani tunayohitaji

    {
    Aa-eh njooni wote
    Aa-eh tusali pamoja
    Aa-eh tuombee amani
    Hatari inatukabili
    Tumuombe Mungu atuepushe
    } * 2

  2. Mizinga maroketi imetayarishwa
    Madege ya kutisha ituangamize
    Ngao yetu wanyonge ... ...
    Yatubidi tusali vita tutashinda
  3. Ujambazi wa kutisha umetuandama
    Mali yathaminiwa kuliko uhai
    Twahitaji ulinzi wa Mungu Mwenyezi
    Aombaye hupewa, njooni tuombe
  4. Ndani ya familia moto unawaka
    Kupigwa tusi mateke sasa ndizo sala
    Watoto nao pia ni vurugu tupu
    Hawana mchungaji kwenye familia
  5. Wito umetolewa tusali rozari
    Baba Mtakatifu anatuhimiza
    Matendo ya rozari tuyatafakari
    Naye Mama wa Mungu atatusikia