Alfajiri ya Kupendeza
Alfajiri ya Kupendeza | |
---|---|
Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
Album | Tazameni Miujiza (Vol 2) |
Category | Offertory/Sadaka |
Composer | J. C. Shomaly |
Views | 46,407 |
Alfajiri ya Kupendeza Lyrics
[ b ] Alfajiri ya kupendeza, ni siku njema siku yenye baraka,
[ w ] Jua limekwishachomoza, laamsha wote waliolala
Ndege nao wanalialia kumshukuru Muumba ( njooni )
{ Njooni baba, mama na watoto
Njoni wote mbele za Bwana
Tumtolee shukrani zetu, kwa kutoa sadaka } *2- [ s ] Ndege wanamshukuru, kwa sauti za kupendeza
Na sisi tumshukuru, kwa zawadi alizotupa (njooni) - Wanyama pia na mimea, vyote vimeumbwa na Mungu
Vitu vyote vya duniani, vyapaswa kumshukuru Mungu (njooni) - Kaiumba dunia hii, kaweka giza pia mwanga
Mchana tufanyeni kazi, usiku na tupumzike (njooni)