Beba Mikononi
Beba Mikononi Lyrics
- Tusimame ndugu twende kwake Bwana (kweli)
Usisite ndugu amka twende hima
Beba mikononi (mwako) uliyojaliwa
Peleka kwa Bwana, upate Baraka
- Peleka kwa moyo, moyo wa mapendo (kweli)
Peleka kwa Bwana uliyojaliwa
- Sadaka ya fedha, fedha za mifuko (ndugu)
Amka upeleke mezani kwa Bwana
- Mavuno mifugo, ni mali ya Bwana (kweli)
Tupeleke kwake atazipokea
- Mkate divai tupeleke kwake (leo)
Tupate baraka mbele zake Bwana
- Twende ndugu twende, mbele zake Bwana (twende)
Tupeleke nafsi zetu kwake Bwana