Hima Hima Najongea
Hima Hima Najongea | |
---|---|
Performed by | St. Francis of Assisi Kariobangi |
Album | Zawadi Tosha |
Category | Offertory/Sadaka |
Composer | Alfred Ossonga |
Views | 13,500 |
Hima Hima Najongea Lyrics
{ Hima hima leo, najongea kwako Bwana,
Ninakuja kwako kwa unyenyekevu wangu,
Nakuletea matunda ya jasho langu,
Pokea Baba nami unipe Baraka } *2- [ t ] Kwa ukarimu nimejitolea mimi mwenyewe,
Polepole nasonga mbele nifike kwako,
[ w ] Nikukabidhi nilicho nacho, hiki kidogo Baba pokea. - Mapato yangu ni duni sana, we wanijua,
Sina kitu kizuri cha kukuletea wewe,
Nakukabidhi maisha yangu, uzima wangu Baba pokea. - Mungu wangu ninakuja kwako nikushukuru,
Umenilinda siku zote asante sana,
Mavuno yangu nakupa wewe, na fedha zangu Baba pokea. - Wiki nzima umenijalia uhai bure,
Umenikinga na matatizo unanipenda,
Mkate huu nakutolea, divai hii Baba pokea. - Baraka zako ninazipokea siku kwa siku
Mungu Baba nionyeshe Mbingu nifanye kazi,
Mifugo yangu nakuletea, furaha yangu Baba pokea.