Login | Register

Sauti za Kuimba

Hima Hima Najongea Lyrics

HIMA HIMA NAJONGEA

@ Alfred Ossonga

{ Hima hima leo, najongea kwako Bwana,
Ninakuja kwako kwa unyenyekevu wangu,
Nakuletea matunda ya jasho langu,
Pokea Baba nami unipe Baraka } *2

 1. [ t ] Kwa ukarimu nimejitolea mimi mwenyewe,
  Polepole nasonga mbele nifike kwako,
  [ w ] Nikukabidhi nilicho nacho, hiki kidogo Baba pokea.
 2. Mapato yangu ni duni sana, we wanijua,
  Sina kitu kizuri cha kukuletea wewe,
  Nakukabidhi maisha yangu, uzima wangu Baba pokea.
 3. Mungu wangu ninakuja kwako nikushukuru,
  Umenilinda siku zote asante sana,
  Mavuno yangu nakupa wewe, na fedha zangu Baba pokea.
 4. Wiki nzima umenijalia uhai bure,
  Umenikinga na matatizo unanipenda,
  Mkate huu nakutolea, divai hii Baba pokea.
 5. Baraka zako ninazipokea siku kwa siku
  Mungu Baba nionyeshe Mbingu nifanye kazi,
  Mifugo yangu nakuletea, furaha yangu Baba pokea.
Hima Hima Najongea
COMPOSERAlfred Ossonga
CHOIRSt. Francis of Assisi Kariobangi
ALBUMZawadi Tosha
CATEGORYOffertory/Sadaka
 • Comments