Naja Mbele Yako

Naja Mbele Yako
Performed by-
CategoryOffertory/Sadaka
Views9,096

Naja Mbele Yako Lyrics

  1. Naja mbele yako ewe Mungu wangu huku nimejawa na dhambi
    Bwana usiniache uniwie radhi, mbele yako Bwana natubu

    Naja kwako nipokee, ingawa mimi nina dhambi *2

  2. Nipe nguvu Bwana nishinde shetani, niishi na wewe daima,
    Nikutumikie siku zangu zote, niking`ara kama theluji
  3. Sadaka naleta ingawa sifai, lakini we Bwana pokea
    Mkate divai zote nazileta, ewe Bwana wangu pokea