Nakuja na Zawadi

Nakuja na Zawadi
Alt TitleNaondoka Mimi
ChoirSt. Anthoney Malindi
AlbumMalindi Kuna Nini
CategoryOffertory/Sadaka
ComposerAlfred Ossonga

Nakuja na Zawadi Lyrics

 1. Naondoka mimi naenda kwa Baba,
  Nipeleke hiki nilichokipata,
  Japo kidogo, sitaona haya,
  Nimeamua, sitarudi nyuma

  { Nakuja polepole Baba,
  Nakuja na zawadi yangu
  Naleta mbele zako ili nitoe shukurani } *2

 2. Natembea mimi mwendo wa madaha,
  Nakanyaga chini kwa maringo tele,
  Naelekea, altare ya Bwana,
  Nimkabidhi, nilichojaliwa.
 3. Nimechangamka ninashangilia,
  Napiga kelele kelele za shangwe
  Nachezacheza, najongea kwako,
  Ee Mungu Baba Nipokee mimi.
 4. Nafsi yangu mimi naileta kwako,
  Mkate divai pia ninaleta
  Uigeuze, mwili na damuyo,
  Chakula chetu, tunaosafiri
 5. Mavuno shambani mimi nimevuna,
  Mifukoni fedha nimekabidhiwa,
  Mimi ni nani, nisikushukuru,
  Baba nasema asante kwa yote.

Favorite Catholic Skiza Tunes