Ndugu Zangu Twendeni
| Ndugu Zangu Twendeni |
|---|
| Performed by | - |
| Album | Viuzeni Mlivyo Navyo |
| Category | Offertory/Sadaka |
| Composer | Basil Lukando |
| Views | 6,847 |
Ndugu Zangu Twendeni Lyrics
- Ndugu zangu twendeni - tukatoe sadaka
Twende kwa moyo safi - tukatoe sadaka
Kwani,
Ukimpa Mungu wako sadaka kwa moyo mnyofu,
Naye,
Naye Mungu atakuwa na neema siku zote.
- Twende kwa ukarimu - tukatoe sadaka
Mkate pia divai - tukatoe sadaka
- Mazao ya mashamba - tukatoe sadaka
Hata na fedha zetu - tukatoe sadaka
- Hata kidogo twende - tukatoe sadaka
Hata na nyoyo zetu - tukatoe sadaka