Nikulipe Nini
Nikulipe Nini Lyrics
- Nikulipe nini ewe Mungu Baba wa Mbinguni
Kwani mtu mimi sina kitu cha kujivunia
Uhai na nguvu ni zawadi nzuri umenipa wewe Baba.
Maisha mazuri ni talanta safi nimepata kwako wewe
Sasa nakuomba baba nigeuze chombo chako
Nimejitolea kwenda kutangaza neno lako *2
- Nikufananishe na nini humu ulimwenguni
Uliumba vyote bahari mito hata milima
- Ningekuwa ndege hakika ningeruka angani
Ningekuwa nyota ningemulika dunia yote
- Nitakutendea nini ili nikufurahishe,
Nitakuimbia wimbo gani Baba nikusifu
- Unitume Baba popote nipeleke ujumbe
Nitalihubiri Jina lako daima milele