Nikupe Nini Ee Mungu

Nikupe Nini Ee Mungu
Performed byMoyo Safi (Unga Ltd)
AlbumNikupe Nini Mungu Wangu
CategoryOffertory/Sadaka
ComposerG. A. Chavallah
Views41,723

Nikupe Nini Ee Mungu Lyrics

  1. Nikupe nini ee Mungu cha kukupendeza
    Uwezo wangu mdogo Bwana waujua
    Pamoja na dhiki inayonisonga
    Pokea zawadi yangu hii duni
  2. Nikitazama wenzangu wanakutolea
    Zawadi nyingi na nzuri za kukupendeza
    Kasoro mimi tu natoa kidogo
    Wakati mwingine sitoi kabisa
  3. Maisha yangu ya dhiki Bwana wayajua
    Unyonge na udhaifu wangu waujua
    Sina kitu mimi cha kukutolea
    Lakini pokea nafsi yangu Bwana
  4. Nayakabidhi maisha yangu kwako Bwana
    Uniongoze katika njia za uzima
    Unisaidie wakati wa shida
    Kwani ni wewe tu tumaini langu
  5. Kutoa ndugu ni moyo sio utajiri
    Ukimtolea Mungu atakuongeza
    Uwasaidie watu maskini
    Wasiojiweza utabarikiwa
  6. Ninawasihi wenzangu mliojaliwa
    Maisha bora mazuri na ya kuridhisha
    Msimsahau Bwana Mungu wenu
    Toeni kwa wingi mtabarikiwa.