Nikupe Nini Mungu Wangu

Nikupe Nini Mungu Wangu
Performed bySauti Tamu Melodies
AlbumZilipendwa
CategoryOffertory/Sadaka
ComposerBasil Lukando
VideoWatch on YouTube
Views51,272

Nikupe Nini Mungu Wangu Lyrics

 1. { Nikupe nini Mungu wangu, nikupe nini we Mwokozi
  Nikupe nini Bwana wangu cha kukupendeza } *2

 2. Kila nitakachoshika mbona bado ni kidogo
  Fadhili unazotenda kwangu mimi naogopa
  Ninakuomba Mwokozi, nifanyie msamaha na unipokee
  Mema unayoyatenda, nitafanya nini mimi nikurudishie
 3. Nakutolea mkate toka mmea wa ngano
  Nakutolea divai ni tunda la mzabibu
  Ninakuomba Mwokozi . . .
 4. Mchana hata siku wewe wanisimamia
  Na nikiwa safarini waniepusha ajali
  Ninakuomba Mwokozi . . .
 5. Nikiwa na matatizo Bwana wanisaidia
  Nikiwa kwenye majonzi Bwana unanifariji
  Ninakuomba Mwokozi . . .
 6. Kama njia siioni Bwana unaniongoza
  Na hata nikipotea kwako unanirudisha
  Nitatoa nini mimi, kitakachokuwa sawa, na fadhili zako
  Nitaimba vipi mimi, niyataje mema yote, utendayo kwangu