Michango Yenu
| Michango Yenu | |
|---|---|
| Alt Title | Sasa ni Wakati Mwafaka |
| Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
| Album | Mshike Mshike (Vol 5) |
| Category | Offertory/Sadaka |
| Composer | J. C. Shomaly |
| Views | 3,934 |
Michango Yenu Lyrics
{ Sasa ni wakati mwafaka wa kutoa sadaka yako ndugu
Hima ndugu jitolee kwa moyo wa ukarimu } *2
Iwe ni fedha pia hata mali umtolee Muumba wako
Akulindaye akuamshaye akupaye hewa na afya njema
{ Waumini, wote tuamke pamoja na sasa tujenge kanisa
Kanisa letu litasitawi kwa michango michango yetu } *2- Kwa moyo wako wa ukarimu mpe muumba wako
Sadaka yako kama shukrani yako
Ujiulize kwa jinsi gani, Bwana kakubariki
Umtolee kama shukrani yako. - Wiki hii nzima amekulinda sasa jifikirie
Ni kitu gani kiwe dhamana yako
Umshukuru kwa jinsi gani naye afurahie
Kwa mema mengi anayotenda kwangu, - Wewe mzima ni wengi sana leo hawaamki
Jifikirie ni wangapi umetenga
Na familia yako daima shida haziwakumbi
Si kwamba hao ni bora kuliko wote.