Sasa ni Wakati Mzuri
Sasa ni Wakati Mzuri | |
---|---|
Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
Album | Ikatetemeka Nchi (Vol 3) |
Category | Offertory/Sadaka |
Composer | F. Mtegeta |
Views | 7,854 |
Sasa ni Wakati Mzuri Lyrics
Sasa ni wakati mzuri twendeni madhabahuni,
Tukatoe sadaka zetu, tulijenge kanisa la Mungu
{ Ewe ndugu yangu mkristu,
Changamka, changamka, peleka sadaka kwa Bwana.
Nenda katoe kwa moyo mweupe
Uzipate baraka za Mungu } *2- Mkristu kutoa sadaka,
Ndio wajibu wa kila mmoja,
Hivyo mkristu kumbuka wajibu,
Nenda katoe sadaka kwa Bwana. - Mwambie Bwana Mungu wako,
Baba pokea nilichokileta,
Hiki ndicho ulichonijalia,
Nakutolea kama shukrani. - Zamani za mababu zetu,
Walipeleka sadaka za nyama,
Nasi wakristu wa leo twendeni,
Tupeleke fedha za mifukoni.