Sasa Wakati Umefika

Sasa Wakati Umefika
Performed bySauti Tamu Melodies
AlbumZilipendwa
CategoryOffertory/Sadaka
ComposerBasil Lukando
VideoWatch on YouTube
Views51,906

Sasa Wakati Umefika Lyrics

 1. Sasa wakati umefika, wa kushika nilicho nacho (mimi)
  Kwa wema niende kwa Mungu nitoe zawadi
  Sasa wakati umefika kwenda mbele ya Mungu wangu (mimi)
  aone nilivyoandaa zawadi ya leo
  Nitamwambia Bwana pokea hiki kidogo nilichonacho
  Kwani Mungu wewe wanijua mimi siwezi hata kueleza
  Nakusihi sana Baba unipokee
  Nigawie na baraka niwe salama

 2. Mema yote niliyokuwa nayo yametoka kwa Mungu
  Hivyo nami ni kosa kusahau, kumshukuru
  Kwani kuwepo hapa leo hii ni kazi ya nani
  Kamwe mimi sitapata uwezo, pasipo Mungu
 3. Mema aliyotenda Mungu nijibu lini na vipi,
  Mbona hofu yazidi kuwa ndani, ya moyo wangu
  Mbele ya Bwana Mungu wangu kufanya siri ni bure
  Yeye ndiye mpanga mambo yote, ya wanadamu
 4. Pumzi inayonipa uhai inatoka kwa nani
  Bila Mungu hakika mwanadamu, siwezi kitu
  Nimepata nafasi ya leo ya kwenda kutoa zawadi
  Heri niende ya kesho sio yangu, ajua Mungu
 5. Ewe mwumba wa vyote duniani na vyote mbinguni,
  mimi leo nakuja kwako Baba, nihurumie.
  Baba we ndiwe unayetawala kulala na kuamka kwangu,
  Juu yangu utake nini Baba, kisifanyike.