Tazama Bwana Tunakuja
   
    
     
         
          
            Tazama Bwana Tunakuja Lyrics
 
             
            
- { Tazama, Bwana tunakuja kwako (leo)
 Twaleta sadaka yetu mbele yako
 Tunakuomba Mungu Baba pokea } *2
- Kwa nguvu zako uliweza kustawisha
 Mazao bora, na sasa twakutolea
 Mashamba uliyarutubisha kwa
 Mvua nzuri mazao kwa wingi yakasitawi
- Bahari mito na maziwa Bwana ukajaza
 Samaki wengi wa kupendeza
 Angani ndege wengi wanarukaruka
 kushangilia neema yako ee Bwana
- Wanyama maporini wanarukaruka
 Kushangilia neema yako ee Bwana
 Wadudu nao wakachecheza kuonyesha
 Furaha kubwa waliyo nayo