{ Tumesisimka (kweli) tunakuja kwako ee Baba
Tumeandama (sote) tunaleta zawadi zetu
Waumini wote simameni twende pamoja,
Tupeleke fedha mavuno na mifugo yetu } *2
- Ondokeni Baba na mama ondokeni nanyi watoto
Chukueni fedha na mali, tupeleke mbele za Bwana
Tuweke akiba mbinguni, nasi tutabarikiwa *2
- Hima hima twende pamoja, hima hima twende kwa Bwana
Tupeleke furaha zetu, tupeleke uchungu wetu
Simameni twende kwa Bwana tupeleke nyoyo zetu
- Fedha za mifukoni mwetu tupeleke kwa ukarimu
Na mapato ya nguvu zetu, tupeleke kama zawadi
Twende kwake tumshukuru, sote tupate Baraka*2
- Mavuno tuliyojaliwa, kutokana na jasho letu
Mifugo tunaowafuga, tupeleke kama sadaka
Tutabarikiwa zaidi, Bwana atatubariki *2
- Mkate mazao ya ngano, divai tunda la zabibu,
Kageuza mwili na damu, tutakula na kubakisha,
Tutapata nguvu zaidi, na uzima wa milele *2
|
|
|