Tunakuja na Vipaji

Tunakuja na Vipaji
Alt TitleTunaleta Mavuno
Performed bySt. Joseph Migori
AlbumNimeteuliwa
CategoryOffertory/Sadaka
ComposerAlfred Ossonga
Views21,354

Tunakuja na Vipaji Lyrics

  1. Tunakuja na vipaji vyetu, mbele zako ee Bwana
    Tunatoa shukurani zetu, kwako Baba Muumba

    Tunaleta mavuno, Bwana Mungu pokea
    Tunaleta na fedha, Bwana Mungu pokea
    Mkate na divai, Twakuomba upokee

  2. Ni matunda ya mashamba yetu, uliyotujalia
    Ndilo jasho letu sisi Bwana, twakuomba pokea
  3. Watumishi wako tunakuja, na zawadi kidogo
    Twakusihi sana Mungu Baba, pokea mikononi
  4. Nafsi zetu zote mali yako, utupokee sisi
    Ee Bwana utujalie afya, uzima na baraka