Twaja Kwako

Twaja Kwako
Performed byOur Lady of Fatima Kongowea
AlbumUninyunyizie Maji (vol. 2)
CategoryOffertory/Sadaka
Views10,459

Twaja Kwako Lyrics

  1. Twaja kwako Baba Mungu na vipaji vipokee *2
    Tu wa dhambi - Baba Mungu twakusihi tupokee.
    Tunaleta - sadaka twakusihi upokee
    Mkate pia - na divai twakusihi upokee *2

  2. Sadaka tunaleta, japo sisi wakosefu,
    Twakuomba Baba Mungu, upokee ni vipaji.
  3. Mkate pia na divai, vyote tunakutolea,
    Vitakase vibariki, twakuomba vipokee
  4. Tunaleta na mazao, ni mazao ya mashamba,
    Kazi ya mikono yetu, twakusihi upokee
  5. Fedha za mifukoni, yote ni mali yako,
    Yote tunakutolea, Baba Mungu upokee.