Upokee Sadaka Yetu
Upokee Sadaka Yetu Lyrics
- Upokee sadaka yetu *2,
Ee Bwana Mungu – twakutolea
Twakutolea – vipaji vyetu, Vipaji vyetu – sadaka kwako
- Upokee sadaka yetu *2,
Ee Bwana Mungu –tunakuomba
Tunakuomba – uzipokee, Uzipokee – sadaka zetu
- Upokee mazao yetu *2,
Ee Bwana Mungu – ni mali yako
Ni mali yako – twakutolea, Twakutolea – mazao yetu
- Upokee na fedha zetu *2,
Ee Bwana Mungu –ni jasho letu
Ni jasho letu – twakutolea, Twakutolea – ni jasho letu
- Upokee na shida zetu *2,
Ee Bwana Mungu – tunakuomba
Tunakuomba – uzipokee, Uzipokee – na shida zetu
- Upokee mkate wetu *2,
Ee Bwana Mungu – ni kazi yetu
Ni kazi yetu – tunayofanya, Tunayofanya – twakutolea
- Upokee divai yetu *2,
Ee Bwana Mungu – ya mizabibu, Ya mizabibu –
tunayopanda, Tunayopanda – kwa shamba zetu