Utukuzwe Ewe Baba
Utukuzwe Ewe Baba Lyrics
- Utukuzwe ewe Baba Mungu utukuzwe, aleluya
Utukuzwe ewe Baba Mungu utukuzwe, aleluya
Utukuzwe - utukuzwe
Baba Muumba ulimwengu - aleluya
- Tumepokea mkate, mazao ya mashamba -
Ndio alama kwetu, ya wema wako mkuu -
- Ni tunda la bidii, ya mkono na ya moyo -
Jalie uwe kwetu, chakula cha uzima -
- Zawadi ya divai, kutoka mzabibu -
Ndiyo alama kwetu, ya wema wako mkuu -
- Ni tunda la bidii, ya mkono na ya moyo -
Jalie iwe kwetu, kinywaji cha kiroho -
- Sifa kwako ee Mungu uliyetuchagua
Shukrani kwako Baba, kwa kutulisha sisi -
- Kwa pendo na fadhili, umetufurahisha -
Ukatufikisha kwa sherehe yetu leo -
- Siku ya leo iwe kwa heshima na sifa -
Na utukufu wako na kwa mafaa yako -