Viuzeni Mlivyo Navyo Lyrics

VIUZENI MLIVYO NAVYO

Viuzeni mlivyo navyo mtoe sadaka
Kwani mnajiwekea hazina mbinguni

 1. Ziwekeni fedha zenu katika akiba ya mbinguni
  Ziwekeni mali zenu katika mifuko ya mbinguni
 2. Msidhani kwamba mnazipoteza mali zenu bure
  Kweli kwamba mnaweka katika hazina ya mbinguni
 3. Viuzeni mali zenu mtoe sadaka kwake Bwana
  Viuzeni vitu vyote mweke hazina ya mbinguni
 4. Rudisheni vitu vyote kwani yeye ndiye aliwapa
  Aliwapa bure nanyi pia mkazirudishe bure
 5. Mkatoe kwake Bwana kwa moyo mmoja na mapendo
  Ni akiba mnaweka katika mifuko ya mbinguni
Viuzeni Mlivyo Navyo
CATEGORYOffertory/Sadaka
 • Comments